Makumi wameripotiwa kuuawa na mashambulizi ya anga ya Israel katika miji ya kusini mwa Gaza

Copyright: HIFADHI ZA TAIFA

Barua
zilizochukuliwa na Jeshi la Wanamaji la Uingereza kabla ya kuwafikia wanamaji
wa Ufaransa wakati wa Vita vya Miaka Saba zimefunguliwa kwa mara ya kwanza.

Ziliandikwa
mwaka wa 1757-8, zilitumwa na wapendwa wao kwa wafanyakazi kwenye meli ya
kivita ya Ufaransa, lakini hazikuwafikia.

Prof Renaud
Morieux, ambaye aligundua barua hizo, alisema zilihusu « uzoefu wa wote wa wanadamu ».

Vita vya
Miaka Saba vilikuwa vita kati ya Uingereza na Ufaransa kuhusu udhibiti wa
Amerika Kaskazini na India.

Ilimalizika
na Mkataba wa Paris, ambao uliipa Uingereza mafanikio makubwa.

Prof
Morieux, msomi wa Chuo Kikuu cha Cambridge, aligundua mkusanyo wa barua 104
kutoka Hifadhi ya Kitaifa huko Kew.

Utawala wa
posta wa Ufaransa uliwapeleka kwenye bandari nyingi nchini Ufaransa ili
kujaribu kuziwasilisha, lakini hawakufaulu.

Meli Galatee
ilitekwa na Waingereza ilipokuwa njiani kutoka Bordeaux hadi Quebec mnamo 1758.

Baada ya
kujua kwamba meli hiyo ilikuwa mikononi mwa Waingereza, mamlaka ya Ufaransa ilipeleka
barua hizo Uingereza, ambako zilikabidhiwa jeshi la wanamaji na mwishowe
zikahifadhiwa.

Maafisa wa
Admiralty wa Uingereza walichukulia barua hizo hazikuwa na umuhimu kijeshi.

Prof Morieux
alisema aliomba tu kutazama kisanduku kwenye hifadhi « kwa udadisi »
kabla ya kuzigundua.

« Niligundua
kuwa nilikuwa mtu wa kwanza kusoma jumbe hizi za kibinafsi tangu
ziandikwe, » alisema.

« Walengwa
wapokeaji hawakupata nafasi hiyo. Ilikuwa nyakati yenye hisia sana, »
alisema Prof Morieux, ambaye matokeo yake yalichapishwa katika jarida la
« Annales. Histoire, Sciences Sociales ».

Zilijumisha barua
kutoka kwa Marie Dubosc kwenda kwa mumewe, Luteni wa kwanza wa meli, Louis
Chambrelan.

Aliandika: « Ningeweza kutumia usiku kucha
kukuandikia … Mimi ni mke wako mwaminifu milele.

« Usiku mwema, rafiki yangu. Ni usiku wa manane.
Nafikiri ni wakati wa mimi kupumzika. »

Watafiti wanasema hakujua mumewe alikuwa wapi au kwamba
meli yake ilikuwa imetekwa na Waingereza.

Hakupokea barua yake na hawakukutana tena, na Dubosc alifariki
mwaka uliofuata kaskazini mwa Ufaransa.

Chambrelan alirudi Ufaransa na kuoa tena mnamo 1761.

Katika barua nyingine, Anne Le Cerf alimwambia mumewe
Jean Topsent: « Siwezi kusubiri kukumiliki. »

« Barua hizi zinahusu uzoefu wa wote wa wanadamu, sio
Ufaransa pekee au karne ya 18, » Prof Morieux alisema.

« Zinaonyesha jinsi sote tunavyokabiliana na
changamoto kuu za maisha. »

« Tunapotenganishwa na wapendwa wetu na matukio
yaliyo nje ya uwezo wetu, kama janga au vita, lazima tujue jinsi ya
kuwasiliana, jinsi ya kuwahakikishia, kujali na kuendeleza shauku.

« Leo tuna Zoom na WhatsApp. Katika karne ya 18, watu
walikuwa na barua tu lakini kile walichoandika kinahisia ya inayofahamika hadi
leo. »

Soma zaidi:

Mashariki ya kati: Jinsi Ufaransa na Uingereza zilivyoigawanya karne moja iliyopita


Crédit: Lien source

Les commentaires sont fermés.