Ufaransa imeanza hatua ya mwisho ya kujiondoa kijeshi kutoka Niger

Mnamo Septemba 24, kutokana na kumalizika kwa ushirikiano wa kijeshi na Niger, Raisa wa Ufaransa Emmanuel Macron aliamuru kurejeshwa kwa wanajeshi wa Ufaransa na vifaa vya kijeshi vya Ufaransa vilivyotumwa nchini humo kwa miaka kumi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Zoezi hilo lilianza Oktoba 5 na linaingi awiki hii katika hatua yake ya mwisho. Wanajeshi  kutoka kambi ya kikosi cha wanaangaanga huko Niamey wanapungua kwa kasi na katika muda wa mwezi mmoja na nusu, hakutakuwa na chochote kitakachosalia kuhusu uwepo wa jeshi la Ufaransa nchini Niger.

Makundi mawili yaliyokuwa yanashiriki katika mapigano na yenye makao yake kaskazini mwa Niger tayari yamekamilisha zoezi hilo la kundoka nchini Niger. Kilichosalia sasa ni kuhamisha kituo chenyewe cha anga cha Niamey. Mwanzoni mwa mwezi Oktoba, kulikuwa na wanajeshi 1,000 ndani ya kami hii, leo wako 400 tu. Na wanajeshi hawa 400 waliingia wiki hii katika hatua ya mwisho ya kuondoka nchini Niger.

Ikiwa helikopta na ndege zisizo na rubani na vifaa vingine vya kijeshi viliwasili nchini Ufaransa siku chache zilizopita, sasa ni muhimu kuhamisha rasilimali za kiufundi za Jeshi la Anga, jenereta za umeme, vipuri na mwishowe miundombinu ya kambi.

Ndge yenye chapa A400M hufanya safari nchini Ufaransa kila siku

Kila wiki, magari ya kijeshi huondoka BAP huko Niamey kwenda Ndjamena, njia pekee ya kutoka kwa wanajeshi wa Ufaransa. Njia ya anga pia inafanya kazi: ndege ya usafiri ya A400m inafanya safari kwenda Ufaransa kila siku.

Zoezi hili lnafanyika kwa utaratibu na usalama na kwa mujibu wa mipango, amebaini Kanali Gaudillière, msemaji wa makao makuu ya jeshi la Ufaransa. Wanajshi hao wameangazia lengo la kukamilisha zoezii hili kabla ya mwisho wa mwezi wa Desemba.

Crédit: Lien source

Les commentaires sont fermés.