Rais Tshisekedi amelaani ghasia dhidi ya mgombea wa upinzani Martin Fayulu

Nairobi – Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, kupitia kwa msemaji wake Tina Salama, ameeleza kusikitishwa na vitendo vya kukosa uvumilivu wa kisiasa, baada ya kinara wa upinzani nchini humo, Martin Fayulu, kushambuliwa kwa mawe wakati akiwa katika mfululizo wa mikutano yake ya kampeni kwenye mji wa Tshipaka jimboni Kasai.

Imechapishwa:

Dakika 1

Kwa mujibu wa Tina Salama, rais Tshisekedi analaani tukio hilo la Novemba 4, na kuwataka raia na wadau wengine kufanya siasa za amani.

Licha ya vurugu hizo, Fayulu alifanikiwa kuendelea na mkutano wake, huyu hapa Prince Epenge, msemaji wa muungano wa Lamuka.

Licha ya kurushiwa mawe umati wa watu ulikusanyika katika eneo la mkutano, tunataka watuambie kwamba ni kwa bahati mbaya, hiyo ilitokea, shambulio la Tshikapa ni jaribio la mauaji. alisema Prince Epenge.

Prince Epenge, msemaji wa muungano wa Lamuka

Raia wa DR Congo wanatarajiwa kuwachagua viongozi wao wapya katika uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba mwaka huu, ambapo wagombea 26 wa urais wameidhinishwa na tume ya uchaguzi CENI kugombea.

Wagombea wa upinzani wameonekana kuishutumu tume ya uchaguzi kutokana na kile wanachosema ni kuwepo kwa njama ya kushiriki wizi wa kura kwenye uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Dénis Kadima, ametangaza kuwa tume yake itasimamia uchaguzi huru na wa haki. © CENI DRC

Licha ya hayo, CENI imeahidi kuongoza zoezi lenye uwazi na haki bila ya kuegemea upande wowote wa kisiasa kuelekea uchaguzi huo.

Kuwepo na na wasiwasi kuwa huenda baadhi ya raia wakakosa kushiriki uchaguzi huo kutokana na changamoto za kiusalama katika maeneo ya mashariki ya taifa hilo.

Crédit: Lien source

Les commentaires sont fermés.