Rais wa Rwanda amteua jenerali mwenye utata kuwa waziri

Video content

Video caption: Tazama moshi ukipaa juu ya jengo baada ya shambulio la risasi la Rotterdam

Polisi wa Uholanzi wamemkamata mtu aliyejihami kwa bunduki ambaye
aliwaua takriban watu watatu katika matukio mawili ya ufyatuaji wa risasi
katika mji wa Rotterdam.

Wanasema mshambuliaji huyo wa kiume, 32, alifyatua risasi katika
nyumba moja kabla ya kuiteketeza, kisha akavamia kituo cha matibabu cha Erasmus
cha jiji hilo siku ya Alhamisi.

Alikuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Erasmus, ambacho kina
uhusiano na hospitali hiyo.

Mwanamke, mwenye umri wa miaka 39, na binti yake mwenye umri wa
miaka 14 waliuawa katika shambulio la kwanza. Mhadhiri wa kiume, mwenye
umri wa 43, aliuawa pia kwa kupigwa risasi hospitalini.

Picha zimeibuka zikimuonyesha mwanaume aliyevalia mavazi ya siri
akichukuliwa kutoka kwenye jengo la
hospitali akiwa amefungwa pingu. Sababu za shambulio hilo hazikujulikana
mara moja.

Mlinzi ambaye anasema kuwa alikuwa wa kwanza kwenye eneo la
tukio aliiambia BBC kuwa ilikuwa siku « ya kushtua ».

« Ilikuwa mbaya, mbaya, » alisema,
akionekana kuchanganyikiwa na hakutaka kutaja jina lake.

Alisema kuwa mtu mwenye bunduki hakuwa
ameingia katika kituo cha matibabu kupitia lango kuu.

Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte
aliandikakwenye mtandao wa kijamii: « Mawazo yangu yanaenda kwa waathiriwa
wa ghasia, wapendwa wao na watu wote ambao wamekuwa na hofu kubwa. »


Crédit: Lien source

Les commentaires sont fermés.