UN yataka kikosi cha MONUSCO kisiharakishwe kuondoka DR Congo

Nairobi – Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatilia shaka, uwezo wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na vikosi vya kikanda kuwalinda raia, iwapo kikosi cha kulinda amani nchini humo MONUSCO kitaondolewa haraka, kama serikali jijini Kinshasa inavyotaka.

Imechapishwa:

Dakika 2

Kumekuwa na kikao cha Baraza hilo kujadili hali ya usalama nchini DRC na mchakato wa kuondoka kwa MONUSCO.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi akitoa hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametaka kuharakishwa kwa mchakato wa kukiondoa nchini mwake kikosi cha kulinda amani MONUSCO ambacho kimekuwa nchini hiyo kwa miaka zaidi ya 20.

Walinda usalama wa Umoja wa Mataifa, wanajeshi wa DRC na vikosi wa EAC wamekuwa wakikabiliana na makundi ya waasi mashariki mwa taifa hilo AP – Moses Sawasawa

Rais Felix Tshisekedi ameitaka Umoja wa Mataifa kuanza kuondoa MONUSCO kuanzia mwisho wa mwaka huu na sio Desemba 2024 kama ilivyopangwa.

Linda Thomas-Greenfield, ni Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.

‘‘Tumesikia serikali ya DRC ikitaka Munsco kwanza kujipanga kabla ya kuondoka na waziri wa DRC ametuandikia barua hapa, tunapongeza hatua ya kuwepo kwa mpangilio unaozingatia kuwalinda raia.’’ alisema Linda Thomas-Greenfield, Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.

Linda Thomas-Greenfield, Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa

Mamlaka nchini DRC imekuwa ikisisitiza kuwa wakati umefika wa taifa kuchukua udhibiti wa nchi yake, huku akikishtumu kikosi hicho kwa kushindwa kumaliza utovu wa usalama, Mashariki mwa nchi yake.

Kiongozi huyo amesema ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umekosa kurejesha amani mashariki ya taifa lake licha ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 25.

Monusco ina wanajeshi zaidi ya elfu kumi na sita nchini DRC na ni ya pili katika ukubwa duniani.

Maandamano yamekuwa yakishuhudiwa kwenye taifa hilo dhidi ya walinda usalama wa MONUSCO
Maandamano yamekuwa yakishuhudiwa kwenye taifa hilo dhidi ya walinda usalama wa MONUSCO © Glody Murhabazi/Agence France-Presse

Walinda amani hao wamekuwa wakituhumiwa hata na raia wa taifa hilo kwa kile wanachodai ni kufeli katika majukumu yao, baadhi ya raia wakionekana kuaandamana wakiwataka waondoke kwenye taifa hilo.

Makundi ya waasi yameendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya raia katika baadhi ya maeneo ya mashariki ya DRC hali ambayo imepelekea kutumwa kwa wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusaidia katika urejeshwaji wa amani.

Crédit: Lien source

Les commentaires sont fermés.