Wakaazi wa Mushaki wameanza kurejea baada ya M23 kuondoka

Nairobi – Wakaazi wa mji wa Mushaki, umbali wa Kilomita 40 kutoka Goma Mashariki mwa DRC , sasa wameanza kurejelea shughuli zao za kawaida, baada ya kuondoka kwa waasi wa M 23 na eneo hilo kudhibitiwa na jeshi la FARDC kwa ushirikiano na lile la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Imechapishwa:

Dakika 1

Nikiwa Kijijini MUSHAKE nimekutana Innocent Chirumwa amabye vita kati ya M23 vilisababisha kifo cha mke wake na watoto wake, hapa amethibisha kwamba amerejea kijijini mwake na kufanya kazi kama kawaida.

Wakaazi waliorejea sasa wanataka ulinzi kuimarishwa zaidi iliwaendelea na shughuli zao © Chube Ngorombi RFI

“Hapa maisha ni ya kawaida, tunafanya shughuli kama Kawaida, lakini hivi tuu majuzi kulikuwa na shida ya wana jeshi wazalendo wakati walikuwa wanaingia hapa mjini walikuwa wanazua wasiwasi ila kwa leo watu wanatulia” alisemaInnocent Chirumwa.

Innocent Chirumwa, Mkaazi wa Mushaki

Wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wale wa FARDC wanaonekana hapa wakiendelea kuwalinda raia, hali ya utulivu ikiendelea kuonekana kwa sasa.

Wakaazi hao wamererejea baada ya waasi wa M23 kuaanza kuondoka kwenye eneo hilo
Wakaazi hao wamererejea baada ya waasi wa M23 kuaanza kuondoka kwenye eneo hilo © Chube Ngorombi RFI

Chirumwa amethibitisha namna maisha yanavyoendelea kijijini Mushaki tangu kujiondoa kwa waasi M23 kijijini humo.

“Tunatembea bila shida, watu wanafanya kazi yao hali ambayo inaonyesha kwamba mambo yataendelea kuwa sawa.” aliongezea kusemaChirumwa.

Innocent Chirumwa, aliyerejea Mushaki

Hata hivyo wakaazi kwenye kijiji hiki wamelitaka Jeshi la Congo kuzidisha jitihada za kuimarisha usalama wilayani Masisi.

“Tunachokiomba ni kuhakikisha usalama zaidi porini,ili tuupate uhuru pia wa kwenda mashambani.” 

Innocent Chirumwa, kuhusu hali ya Mushaki

Haya yanajiri wakati huu hali ya utulivu pia ikiaanza kuripotiwa wilayani Masisi.

CHUBE NGOROMBI /GOMA/ RFI KISWAHILI

Crédit: Lien source

Les commentaires sont fermés.